1 Kings 7:1-6

Sulemani Ajenga Jumba Lake La Kifalme

1 aIlimchukua Sulemani miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 2 bAlijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,
Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.
upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,
Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.
likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa.
3Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu. 4Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. 5Milango yote ilikuwa na miimo ya mstatili, ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana.

6 eAkajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini
Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoning’inia.

Copyright information for SwhKC